Thursday, August 10, 2017

Ndoa/familia ina matatizo hayaishi??

Familia ni kitu cha msingi sana katika jamii na ni hakika kuwa bila kuwa na utaratibu wa baba na mama kukaa pamoja wakazaa na kutunza watoto wao basi ni hakuna ustaarabu na huwenda watoto wengi wangekuwa wanawajua mama zao kuliko baba zao.
Kusingekuwa na tofauti kubwa kati ya wanyama na wanadamu katika upande huu kwasababu wote ni wale wale.
Familia inaundwa kwa baba, mama ,na watoto. Lakini tujiulize je nyumba zenye baba na mama mgumba au haijapata mtoto sio familia hata kama ina miaka 40?..
Basi ni wazi kuwa familia inaanzia kuitwa jina lake baada ya mwanaume na mwanamke wanapoanza kuishi pamoja kindoa (wakijulikana kama wanandoa, aijalishi wamefunga ndoa ya kiserikali, kidini au kitamaduni).
Mara nyingi familia hukumbana na matatizo sana na hasa takwimu zinaonesha kuwa ndoa nyingi huingia matatizoni mwaka wa2 mwaka wa 5 mwaka wa12 na mwaka wa 20 n.k.
Japo uzoefu unaonesha kuwa ndoa nyingi huanza kwa umoto mwingi sana wa raha na furaha hupitia kipindi cha katikati (miaka ya 20) hapo matatizo hupamba moto na kufikia miaka ya 30 ambayo wanandoa hawa huwa na rika ya miaka50/50 hvi ndipo ndoa hutulia na uzee uingia.

Sababu za matatizo katika ndoa nyingi
Kuna sababu nyingi sana za matatizo katika ndoa lakini zote hiwezwa kugawanywa makundi mawili (2) ambayo ni
1. Sababu za ndani ya ndoa
2. Sababu za nje ya ndoa

Nikianza na namba 1. Sababu za ndani ya ndoa hizi nimeziingiza sababu ambazo husababishwa na wanandoa wenyewe ikiwemo :
*kutoridhishana
*jeuri
*kuzoeana na kuonana kawaida kawaida tu.
*tamaa za wanandoa dhidi ya watu nje ya ndoa.
*ukali uliopita kiasi
*chakula kibaya
*ubahili
*kutoijali familia pia.

Sababu hizi na nyinginezo (sio lengo la post) huambatana sababu za nje ya ndoa na wakati mwingie zenyewe tu huitetelesha ndoa.
2. Sababu zA nje ya ndoa
Sasa hizi ni zile ambazo huanzia katika jamii inayowazunguka wanandoa hao. Hizo sasa ni
1. Ukoo kumkataa mwanandoa mmoja.
2. Jamii kuichukia familia yenu
3. Ugumu wa maisha n.k
4. Umbea na maneno ya uongo.
* hizi maranyingi huweza kuingia ndani ya ndoa na kuitetelesha kwa sababu ya uzembe tu miongoni mwa wanandoa hao. Wao kushindwa kujisimamia na kuchukua kila kitu kama kilivyo basi ndio huwaaribia ndoa

Lakini ndoa inapoyumba unahitaji kufanya nini?????
Ni dhahili kuwa ndugu mpenzi msomaji wa princemarawa blog yako ya kijamii inayokupa burudani na raha tele ya muziki huku ukiendelea na mambo mengine .
Basi ndoa yako inapoyumba wewe kama mwanandoa unahitaji kufanya nini. Basi fanya mambo yafuatayo.
Kama wewe ni mwanamke basi fanya haya:
Mfate na mwulize mmeo kwa upole juu ya jambo ambalo ni tofauti na liloloyumbisha familia yenu. Ongeleeni jambo hilo mpaka utakapomwona mmeo anaonekana ana morari au yuko kawaida kabisa (in normal mood ) kisha taratibu hamishia mjadala kwenye suala ambalo limeyumbisha familia yako na muongee kwa undani na kuishia kumwomba msamaha na kukiri kuwa wewe umekosea hata kama yeye amekamatwa ugoni 😀😂😁.
Yap pana ugumu hapo ila ndio utakuwa unaiponya ndoa yako kwa namba hiyo. Kisha mwishoni mwambie mme wangu tuwe waaminifu tu katika famila yetu tujenge maisha.
Usimgusie suala alilokamatwa nalo (kosa) UGONI, kwsbb kufanya hivyo utakuwa umeharbu hata msamaha wako utageuka kuwa kichapo vha mbwa mwitu yani na utaona princemarawa imekutafutia pili pili kichaa kwenye ndoa yani.
Mwanamke wewe unahitaji kuwa na busara zaidi na hekima pia uvumilivu na kiasi ndio ndoa yako utaiponya na kuifanya isonge mbele.
Moja ya wajibu wa mwanamke ni kupokea kila mkiki unaotokea ndani ya ndoa na kuuzima ( kuwa shock absorber )
Mwanamke ndiye huibariki familia na kuifanya isisambae sambae hovyo. Hata siku moja mama usijaribu kunyanyua kamdomo kako ka leap stick nyekundu na meno ya whitedent kumkanya mmeo kwa kumwambia kosa lake moja kwa moja au kwa kumkaripia utaumia .
Mwanamke kama alivyo mwanaume pia wote wanapendw kuambiwa na kukanywa kwa upole na upendo huku akibembelezwa japo ameacha tsh elfu1 ila anataka wali wa nazi na samaki sato wa karanga na hoho he he he.
Si mtoto,si mdada,wala mmama au mbaba wote huwa wanapendwa kukanywa kwa upole,upendo ila hakikisha kabla ya kumwambia mtu kosa lake umjengee mazingira mazuri ya kumwambia. UnaweZ ukamfanyia mkeo surprise akafurahi sana kisha ukamwambia mke wangu nimefurahi sana kwa kile na hiki na kile kule yani ndio maana hata nimeamua kukuzawadia hii surprise lakini kweli moja mbili na tatu hizi ulinikwaza sana ila kwakuwa u mke wangu basi yaishe na usiyarudie basi hakika katka furaha na upendo huo mke au mmeo atarekebishika.
Baba familia si ulingo au sehemu ya kuoneshea misuli n uwezo. Ni chuo cha msahama, furaha na upendo. Na hakika kama mke au mmeo ungekuwa unakaa naye kwa magumi na ubabe kipindi cha kampeni basi hakika asingekubali kukaa na wewe ila ulimwonesha furah, raha na upendo akapenda kuishi na kuwa tayari hata kukuambia nitakufa na wewe tu😂.
Msingi wa ndoa ni furaha na upendo tu wala si pesa na mamlaka.
Familia inataka demokrasia zaidi na ukumbuke kuwa
*matatizo ya familia huwa yanatatuliwa na wanafamilia wenyewe wala si shangazi dada au bibi au mahakama na wanasheria au majilani

Dura makabila -demu wangu namba ngapi